elru87tYGBGEm Soko Maarufu Kenya la Gikomba Nairobi Laungua na Moto - EDUSPORTSTZ

Latest

Soko Maarufu Kenya la Gikomba Nairobi Laungua na MotoMoto umechoma upande mmoja wa soko la Gikomba jijini Nairobi na kuharibu mali ya thamani isiojulikana mapema Jumatatu. Saa 48 kabla, wafanyabishara walipata pigo baada ya huduma ya jiji la Nairobi kupatiwa ruhusa na mahakama kuwaondoa baadhi ya wauzaji mitumba ili kutoa nafasi ya upanuzi wa kituo cha afya cha Pumwani Majengo Health Center.Eneo la soko lililochomeka lilikuwa lile la mitumba ambapo wafanyabiashara wengi uhifadhi mali yao.

Wafanyabiashara waliowasili walikuwa tayari wamechelewa kuokoa mali yao huku ikiwa ni mabati yaliochomeka pekee ndio yaliosalia.

Gari la huduma ya Zima moto la jiji la Nairobi liliwasili katika eneo la tukio lakini moto huo tayari ulikuwa umesambaa kutokana na vibanda vya mbao vilivyotengenezwa .

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz