Harmonize "Nilitaka Tupatane Au Nilipe Pesa Niwe na Amani" - EDUSPORTSTZ

Latest

Harmonize "Nilitaka Tupatane Au Nilipe Pesa Niwe na Amani"“Nikamwambia Boss Kusaga, akasema nimuonyeshe mkataba wangu, nikamuonyesha akasema mkataba huo una vitu vingi na hata akinitafutia mwanasheria siwezi kulipa fedha.

“Nikamwambia sitaki anitafute mwanasheria, kuna mambo mawili, aongee na bro tukayamalize au au nitafute njia ya kulipa fedha za kuvunja mkataba.

“Ninachotaka mimi ni amani, akasema atanirudia, ila hakunirudia, nikasema hapa nimekosa msaada.

“Nikamfuata mama yake Nasib, mama Dangote, nikamueleza kuwa kuna vitu siridhiki navyo.

“Tumetoka mbali na bro, sikutaka kuondoka vibaya, nilitaka nimfanye yeye awe nguli wa muziki Afrika, afeel proud kunisainisha mimi.

Kauli za Harmonize baada ya kutua Dar es Salaam, leo Alhamisi akitokea Marekani.”

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz