Harmonize "Diamond Platnumz Alisema Simuwezi Kihela, Serikali na Kiuchawi" - EDUSPORTSTZ

Latest

Harmonize "Diamond Platnumz Alisema Simuwezi Kihela, Serikali na Kiuchawi"




MWANAMUZIKI Harmonize, jana Alhamisi, Novemba 18, 2021 amerejea nchini akitokea Marekani alipokwenda kufanya shoo zake baada ya kutua nchini ameongea na wanahabari katika Uwanja wa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kueleza sababu zilizosababisha yeye kuondoka katika Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) iliyo chini ya Diamond Platnumz.

“Nilimfuata Diamond nikamwambia tatizo ni nini mimi na wewe tunagombana? Akasema hivi: ‘Mimi nikimpa mtu heshima yangu, kama hatanirudishia naichukua kinguvu, unataka kushindana na mimi huniwezi kihela, huniwezi kiserikali, huniwezi kichawi nipe mkono tushindane’.

“Nikabaki nimezubaa, akaingia kwenye gari akaondoka. Siku iliyofuata nikaenda ofisini kwake kumuona.”

“Wakati Wasafi inaanzishwa mimi na yeye ndiyo tulikuwa tunapambania Wasafi, nilikuwa kimbelembele kusimamia vitu vingi, hata baadhi ya vifaa nilitoa mimi baada ya vya kwake kuchelewa.

HABARI KAMA  HIZI UNAZIPATA KUTOKA APP YA UDAKU SPECIAL PEKEE  DOWNLOAD  HAPA UWE NAYO KWENYE SIMU YAKO

“Kamati ilikuwa mimi yeye, Mustapha na mama Dangote, wakati huo hakukuwa na Babu Tale wala Sallam, wao walikuwa bize na Dizzim, kwa walikuwa hawaamini kwenye Wasafi Media.” amesema Harmonize.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz