Baba Levo Amjibu Babu Tale "Mwambieni Babu Tale ni Mpumbavu" - EDUSPORTSTZ

Latest

Baba Levo Amjibu Babu Tale "Mwambieni Babu Tale ni Mpumbavu"
Mbunge wa Morogoro kusini Mashariki, @babutale ametaka wadau/mashabiki wa muziki kuwaondoa/kuwapuuza watu wachache kama @officialbabalevo , @mwijaku_01 na Juma Lokole ambao wanaharibu image ya huu muziki,badala ya kupatanisha wao furaha yao ni kugombanisha.

Hasa Kupitia ukurasa wa Sam Misago, Baba Levo ameenda kucomment kwenye clip hiyo ya Babu Tale na kutaka watu wakamwambie Babu Tale kuwa yeye ndiye mpumbavu.

Ikumbukwe Babu Tale pia aliwahi kukemea watu waliokuwa wakikebehi na kubeza show za @harmonize_tz
Alizokuwa akifanya Nchini Marekani, na hata Harmonize amewahi kukiri kuwa hawezi kutana na Babu Tale akampita bila salamu, maana ni mtu ambaye hana unafiki wala mikunjo.

Kwa mtazamo wangu, ifike hatua B Levo ujitathimini sana kwenye hili, mwisho wako ni mfupi sana ikiwa majivuno haya yataendelea kuvuka mstari, maana wewe si wa kwanza kufanya kazi na @diamondplatnumz na hautokuwa wa mwisho pia. Diamond ana tabia moja akikupa mgongo ndio imeisha hiyo, nadhani mifano ipo ya akina  Q Boy msafi, Kifesi, Dudu Baya na wengineo waliowahi kuwa karibu na Diamond. Hawezi vumilia kuona unawavunjia heshima hadi maboss zake na akakuchekea.

@sajomedia
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz