Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Zuchu toka Januari hadi Septemba mwaka huu amekuwa ndiye msanii wa kike anayeongoza kutazamwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube nchini Tanzania.
Kwa kipindi chote, Zuchu amekuwa akipata views zaidi ya milioni 10 kila mwezi ambapo Februari ndipo alipata views wengi zaidi ikiwa ni zaidi ya milioni 25.
Zuchu ambaye alisainiwa WCB Aprili 2020, mwaka huu aliweka rekodi ya kuwa msanii wakwanza wa kike Tanzania kufikisha views zaidi ya milioni 100 YouTube.
Utakumbuka Januari mwaka huu Zuchu aliachia wimbo wake 'Sukari' ambao video yake imeweza kufikisha views zaidi ya milioni 50 na ndio video pekee iliyotoka mwaka huu Tanzania na Afrika Mashariki yenye views wengi YouTube.
No comments:
Post a Comment