Watatu Wakamatwa kwa Mauji ya Mtendaji Dar - EDUSPORTSTZ

Latest

Watatu Wakamatwa kwa Mauji ya Mtendaji Dar
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mtendaji wa mtaa wa Mbezi Msumi, aliyejulikana kwa jina la Kelvin Costa Mowo (38), wakati akitekeleza majukumu yake ya kusikiliza wananchi ambao walikuwa na mgogoro wa ardhi.

Kelvin aliuawa dunia jana Jumatatu, Oktoba 11, 2021 majira ya saa 5:54 baada ya watu wasiojulikana kumvamia ofisini na kuanza kumshambulia kwa mapanga mpaka kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa wengine bado wanasakwa ili kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz