Ukweli Kuhusu ‘Pisi Kali’ ya Sabaya Mahakamani



BAADA ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake watatu kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha au unyang’anyi wa makundi (gang robery), mambo yamezungumzwa, lakini kubwa ni mrembo anayedaiwa kuwa ni mchumba wa jamaa huyo.

Picha ya mrembo huyo mkali; kimjinimjini wanamuita ‘Pisi Kali ya Sabaya’, imeendelea kusambaa ikisemekana kwamba, ndiye mchumba aliyelipiwa mahari na Sabaya ambaye alitarajia kuolewa baadaye mwaka huu.

Ilisemekana mrembo huyo ni Mnyarwanda mwenye umbo refu na namba nane huku akiwa na dimpoz za hatari na rangi adimu ya ngozi yake na kumfanya kuwa ‘mtamu’ kwelikweli.

KISA UTETEZI WA SABAYA

Hii ni baada ya Sabaya kutakiwa kujitetea mahakamani ambapo alisema ana mchumba ambaye tayari amemlipia mahari na anatarajia kufunga naye ndoa hivyo baadhi ya watu kuwa na shauku ya kumjua mchumba wake huyo.


Sasa; kwa mujibu wa mrembo huyo ambaye anafahamika kwa jina moja maarufu la Rusaro ni kweli ni Mnyarwanda, lakini hata yeye anashangazwa na habari hizo zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

RUSARO: FAKE NEWS

Kupitia Insta Story yake, Rusaro aliweka picha yake iliyounganishwa na picha ya Sabaya na kuandika; “Fake news…”

Baadhi ya mitandao ya Rwanda imeeleza kuwa, Rusaro aliwashtua wafuasi wake kwenye mitandao ya kijamii wakimuuliza kumbe yeye ndiye aliyelipiwa mahari na anatarajia kuolewa na Sabaya?


Mtandao mmoja umeripoti kuwa, Rusaro amefunguka kwamba, hajui chochote na yeye mwenyewe anashangazwa na jambo hilo na hajui ni nini kinaendelea.

Kwa wanaomjua Rusaro wanasema ni kweli ni pisi kali mno anayeishi Kigali; Mji Mkuu wa Rwanda ambaye amemaliza chuo kikuu mwaka jana.

Hata hivyo, wanasema amezaliwa na kukulia nchini Rwanda na hajui hata Kiswahili na ana mchumba wake ambaye ni mchezaji wa kikapu katika Ligi ya Rwanda.

MCHUMBA HALISI WA SABAYA

Kuhusu mchumba aliyelipiwa mahari, ni yule anayeonekana kwenye video ya Global TV Online ambaye Sabaya alikuwa akimpa busu la mbali baada ya kuhukumiwa.

Mwanamke huyo ambaye ndiye mchumba halisi wa Sabaya anaonekana kwenye video hiyo akiwa mahakamani na mama anayedaiwa ni mama mzazi wa Sabaya na ndugu wengine wa jamaa huyo.

WATU WAWE MAKINI

Kutokana na usumbufu alioupata mrembo huyo wa Kinyarwanda, wataalam wa mitandao ya kijamii wanasema kuwa, ni vyema watu hasa wenye kurasa zenye watu wengi kwenye mitandao ya kijamii na makundi ya WhatsApp wakajitahidi mno kuwa na uhakika wa kile wanachokiposti.

Hata hivyo, kisheria ni kosa kupostim picha ya mtu kwa jambo ambalo linakuwa halina uhakika au ukweli.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post