Nina mdogo wangu wa kike, ni wa mwisho kwetu kuzaliwa, amemaliza chuo miaka 2 iliyopita hakua amepata kazi, amekua nyumbani tu muda wote huo. Kwa kweli for the past two years nimetembea sana kwenye mashirika mbali mbali kumtafutia kazi bila mafanikio. Hadi ilipofika December mwaka Jana nilipomlilia hali bosi mmoja ambae tuna muingiliano wa kikazi katika mashirika yetu.
Mimi huenda kwenye shirika hilo kila mwisho wa mwezi kwa mambo yahusuyo hesabu za shirika za mzee huyu mwenye roho nzuri, akaongea na HR manager wa hapo na hatimae mdogo wangu akaingia kazini baada ya mchujo wa karibu watu 1500 katika mtihani wewe kuandika baadae oral kwa kweli ilikua muujiza.
Sasa amebakiza wiki moja amalize probation, miezi miwili iliyopita bosi wake alimwomba uhusiano na mdogo wangu akamkataa akamwambia yeye ana mtu wake, yule bwana hajakata tamaa ameendelea kumkumbushia jambo hilo binti hadi sasa yule bwana kuona hali imeshindikana akamuita na kumwambia wazi kwamba kama unakataa ombi langu basi sitalipeleka jina lako kwa ajili ya confirmation, akasema anayo sababu nyingine ya kisheria ya kutom confirm.
Hivyo kazi yake ipo hatarini, sasa amelileta rasmi kwangu kuona tunafanyaje kuokoa hii hali, mimi nikamwambia akubali tu kuwa nae haitampunguzia chochote, nikamshauri wazi tu kwamba maisha wakati mwingine ni lazima ujitoe sadaka mwenyewe, watu wote waliofanikiwa wamepita njia ngumu sana na hata wakikueleza huwezi amini ni siri ya mtu moyoni.
Nimejaribu kumpa mifano mingi ya wanawake waliofanikiwa na anaowaona wamekalia viti vikubwa asilimia tisini ni pichu
Lakini binti kasema yeye hawezi kufanya hivyo acha akose tu kazi kwamba ana mtu wake. Kwa kweli nimekasirika sana kwa kitendo hicho, yule mzee alienisaidia pia anaungana nami kwa hili, sasa basi nimemwambia binti kama akipoteza hiyo kazi kwa ujinga wake sitaki kumuona hata kwangu, arudi kijijini kabisa kwa wazazi, maana amewapigia simu kama vile kunisemea vibaya kwa ndugu mbali mbali.
Huyu mtu wake mwenyewe ni fake balaa, huwa tunakutana sana mjini humu akiwa na magumashi kibao sema tu namna gani vipi mambo ya kiume, ana faulo kibao tu. Yaani kwa kweli nimekasirika sana, mimi mwenyewe kazini kwangu nakimbilia hadi begi la bosi wangu kwenye gari asubuhi akifika kama mtoto, yote hiyo ni kujipendekeza ili mambo yaende. Mwaka juzi kuna bosi wangu mwanamke mbaya wa sura kama nini, mumewe alikua na kisukari, kila watu wakiondoka tunajifungia ofisini, lakini nilivumilia hadi alipohamishwa na sasa hivi naishi poa kazini, yote ni kulinda kazi.
Sasa najua wazi huyo bosi wake atatekeleza hicho kitisho anachotoa, hr siku zote wanapokea mapendekezo kutoka kwa line manager, akisema staff huyu ameshindwa probation HR hawezi kufosi, na hii mbinu inatumika sana hasa kwa new comers, huwezi kuruka, labda Mungu akusaidie usitongozwe na bosi yoyote.
Leiza
No comments:
Post a Comment