Mwimbaji Queen Darleen "Kwenye Mziki wa Bongo Mimi ni Nungunungu au Karunguyeye" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mwimbaji Queen Darleen "Kwenye Mziki wa Bongo Mimi ni Nungunungu au Karunguyeye"


Mwimbaji Queen Darleen anasema ameshindwa kujipa jina la mnyama kutokana yale makubwa na yanayosifika yameshachukuliwa na kama kutakuwa na ulazima wa yeye kufanya hivyo, basi atatumia jina la Nungunungu au Karunguyeye.

"Unajua kila anachofanya msanii ana lengo lake, kuna shabiki muda mwigine hajisikii kukuita Queen Darleen, anataka tu kukuita Nungunungu, kwa hiyo inaleta ladha fulani," amesema Darleen.

Baadhi ya wasanii wanaotumia majina ya wakali ni Diamond Platnumz (Simba), Harmonize (Tembo), Rayvannny (Chui), Country (Fisi), Dubu Baya (Mamba) na Afande Sele (Simba).


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz