Baada ya Jana Kupigwa Kimoja Taifa Stars kuwafuata Benin leo - EDUSPORTSTZ

Latest

Baada ya Jana Kupigwa Kimoja Taifa Stars kuwafuata Benin leo





LEO Oktoba 8 Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, inatarajia kuondoka leo saa 6 mchana kuelekea Benin kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Kombe la Dunia.
Jana, Oktoba 7, Uwanja wa Mkapa, Taifa Stars ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na kupoteza pointi tatu muhimu.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2021 nchini Benin ikiwa ni vita ya kusaka pointi tatu muhimu.

Taifa Stars itaondoka na Ndege ya Air Tanzania leo na ina matumaini makubwa ya kuweza kupata ushindi licha ya kuwa mchezo huo utakuwa mgumu.

Kocha Mkuu wa Stars, Kim Poulsen amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kusema kwamba walipata nafasi na kushindwa kutumia ambazo walizipata.

"Tulishindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata hivyo kwa ajili ya mchezo wetu ujao tutapambana kufanya vizuri na kupata pointi tatu muhimu," .

Kwenye Kundi J vinara ni Benin wakiwa na pointi 7 huku Tanzania ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake ni nne.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz