- EDUSPORTSTZ

Latest

MWANAMAMA wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel amefunguka juu ya madolari ya Kimarekani zaidi ya 2,000 (zaidi ya shilingi milioni 4.5 za Kitanzania) alizommwagia Zamaradi Mketema kwenye sherehe yake ya kuzaliwa aliyoifanya nyumbani kwake, Bunju jijini Dar, hivi karibuni.

 

Aunt ambaye ni mama wa watoto wawili ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, anawashangaa watu wanavyosema amepata wapi pesa za kumtunza mtangazaji huyo, wakati ni mambo ya kawaida kwenye maisha yao ya kila siku hivyo watu wakae kwa kutulia.

 

“Kwetu sisi hayo ni mambo ya kawaida sana, sijui nisemaje kwa kweli, kutunzana siyo ishu kwetu ila nashangaa baadhi ya watu wanajadili na siyo kwamba tumeanza leo,” anasema Aunt ambaye alivunja rekodi kwenye kitunza.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz