Mapya yaibuka..Mwanaume Afunga Ndoa na Sufuria la Kupitikia Wali - EDUSPORTSTZ

Latest

Mapya yaibuka..Mwanaume Afunga Ndoa na Sufuria la Kupitikia Wali


Mapya yaibuka ! Pichani Khoirul Anam mwanaume wa nchini Indonesia amefunga ndoa na rice cooker hilo ili liwe mkewe wake. Ndoa imefungwa tarehe 20 September 2021 ambapo bwanaharusi huyo alivaa mavazi rasmi na kupewa cheti cha ndoa kwa kuoa chombo hicho cha umeme kinachotumika kupikia wali. rice cooker hilo lilivalishwa mtandio katika siku hiyo muhimu kwa kwenda kuanza mapya ya ndoa

Khoirul Anam amesema yeye ni mweupe(fair), hapendi kuzungumza sana na pia anapenda kupika na amelipenda sana rice cooker hilo na kuamua kulioa kabisa liwe mke wake huku akilimwagia mabusu ya upendo

Baada ya ndoa hiyo iliyoowaacha watu midomo, jamaa huyo alijitosa mitandaoni kupost picha za siku yake hiyo muhimu kwa kufunga ndoa ingawa bado hajapost picha zao za fungate(honeymoon) na mkewe huyo
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz