Wema Sepetu Jua Limeshazama.. - EDUSPORTSTZ

Latest

Wema Sepetu Jua Limeshazama..




Na @mkisijr

Siku zote katika nchi yetu pendwa ya Tanzania, jua linachomoza upande wa Mashariki na kuzama Magharibi.

Watu mbalimbali uutumia upande wa Magharibi sehemu ambayo jua linazama kama sehemu ya mwisho wa kitu fulani.

“Jua ndiyo lishazama hivyo.” Au utasikia; “Magharibi hiyoooooo.” Misemo imekuwa mingi sana huku wengi wao wakimaanisha jambo ambalo limekwisha muda wake au limepitwa na wakati.

Septemba 28 kila mwaka huwa na kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa aliyewahikuwa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Abraham Sepetu.

Unapolitaja jina la Wema Sepetu, lazima kichwani ijengeke picha ya Wema msanii wa maigizo, mwanamitindo na mjasiriamali.

Amewahi kupamba kurasa za mbele za magazeti pendwa kwa skendo mbalimbali kiasi cha kipindi fulani miaka kadhaa nyuma alivamia kampuni fulani ya magazeti pendwa na kusababisha tafrani za hapa na pale!

Hapa tunamzungumzia Wema wa miaka ya 2000 hadi 2015. Wema alikuwa miongoni mwa ‘Wadada’ maarufu Tanzania. Alikuwa "moto". Kipindi hiki ilikuwa kila msanii wa kike anapenda kuwa na urafiki na Wema, ilikuwa ni bonge la ‘deal’ kuwa na ‘uswahiba’ na Wema.

Kipindi hicho ilikuwa wiki moja kabla ya kumbukizi ya kipenzi hicho cha Watanzania, Dar es Salaam inatikisika. Birthday ya Wema imefika. Umaarufu wa Wema ulikuwa mkubwa mno hadi kupachikwa jina la ‘Tanzania Sweetheart’.

Jana Septemba 28, 2021 ilikuwa birthday ya Wema Sepetu. Inaelezwa ametimiza miaka 31 ya kuzaliwa.

Wema wa jana kweli siyo wa juzi! Wema wa juzi nani asiweke ‘bando’ kumposti na kuandika ‘caption’ taaamu ya kumtoa nyoka pangoni kumsifia mlimbwende huyo wa mwaka 1990? Kila mtu alijisikia fahari kumposti, lakini jana, aaaaah! Wema jua limezama!

Siku kama ya jana, kwa miaka 10 iliyopita ingekuwa siku yake. Kwenye mitandao kusingekuwa na Manara, Mo wala kelele za Simba na Yanga.

Ingekuwa Wema’s Day. Jana hadi kufikia saa sita usiku ni aibu hata kuandika idadi ya watu ambao walimposti mrembo huyo ambaye hadi sasa anapoingia ‘location’ utapenda kazi yake.

Unadhani wapi Wema ameteleza kiasi cha kupungua kwa umaarufu wake kama ilivyokuwa miaka kadhaa nyuma? Kipi afanye arudi kuwa Wema yule? Tupe maoni yako Wema atasoma.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz