Irene Uwoya "Starehe Ninazo Kula na Sehemu Ninazo Enda Bado tu Kwenda Mbinguni" - EDUSPORTSTZ

Latest

Irene Uwoya "Starehe Ninazo Kula na Sehemu Ninazo Enda Bado tu Kwenda Mbinguni"KWENYE haya maisha, mtu anaweza kufanya kila kitu hadi akafikia hatua ya kutamani kwenda mbinguni! Hicho ndicho kinachotokea kwa supastaa wa Bongo Movies, Irene Uwoya ambaye kwa sasa ndiye mwenye mkwanja mrefu mjini.


Uwoya anasema kuwa, kama ni kutembea sehemu za kifahari duniani, ameshafika nyingi tu na bado anaendelea kwenda sehemu mbalimbali kula bata, kiasi kwamba kilichobaki labda ni kwenda mbinguni tu.


Akizungumza na Ijumaa, Irene ambaye hivi karibuni alipanda juu mwinguni na helkopta na kushuka na parachuti,alisema mchezo huo ulikuwa ni ndoto yake kubwa sana lakini anamshukuru sana Mungu,amefanikiwa na bado atazidi kutalii.


“Yaani sehemu ambayo sitafika kwa sasa ni mbinguni labda wakati ukifika,lakini nitatembea sana huku na kule mpaka nimalize kutalii kwakweli” alisema Uwoya.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz