Fahyma Acharuka "Sitaki Kusikia Mambo ya Paula na Msiniulize" - EDUSPORTSTZ

Latest

Fahyma Acharuka "Sitaki Kusikia Mambo ya Paula na Msiniulize"BABY mama wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Shaban Mwakyusa almaarufu Rayvanny, Faima Msenga au Fahyma ametoa msimamo wake kwamba hataki kuulizwa au kutakiwa kuzungumzia uhusiano wa jamaa huyo na mpenzi wake mpya, Paula Kajala.


Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Fahyma ambaye ni mwanamitindo wa kimataifa anasema kuwa, atazungumza juu ya ishu hiyo pale atakapokuwa tayari.


Fahyma anasema kuwa, yeye siyo mtu wa madrama hivyo anaamini mashabiki wake wanahitaji kusikia zaidi kazi zake kuliko hayo mengine hivyo anawaomba waendelee kumsapoti kwenye kazi zake.

 

“No comment, sitaki kusikia au kuzungumzia hayo mambo (ya Paula) kabisa mpaka pale nitakapokuwa tayari mimi mwenyewe kwa sababu kwanza mimi siyo mtu wa drama.

 

“Ninachowaomba mashabiki wangu waendelee kusapoti biashara zangu na kazi zangu zote kwa jumla,” anasema Fahyma ambaye amezaa na Rayvanny mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydany kabla ya jamaa huyo kunyakuliwa na Paula.

STORI; MEMORISE RICHARD, DAR

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz