elru87tYGBGEm Gigy Money na Umber Lulu Wakiwa Serious na Mziki Watatoboa - EDUSPORTSTZ

Latest

Gigy Money na Umber Lulu Wakiwa Serious na Mziki WatatoboaUwenda hawana njaa ya kushindana kimuziki na aina ya maisha wanayo jaribu kuishi ndio upelekea jamii inawachukulia kawaida sana. @gigy_money_og na @iamamberlulu ni wasanii ambao kama wataamua kuwa serious kwenye muziki basi naamini kuna nafasi yao kubwa sana,wana vipaji halisi na ukiangalia muziki wetu hauna wasanii wengi wa kike.

Nampa Papa ilimtambulisha vizuri Gigy Money kwenye muziki na baada ya hapo akaachia Mawe kadhaa yakabamba,sawa kwa Amber Lulu ambaye miaka 4 iliyopita alijitambulisha vizuri na wimbo wa WATAKOMA akimpa shavu @countrywizzy_tz goma likawa lit,Amber Lulu kaachia Amapiano kama una Shingapi ambayo ni moja ya nyimbo bora za Amapiano zilizowahi kufanyika Bongo, Nimeachika remix imekamata zaidi kuliko Nimeachika Og na hasa verse ya Amber ndio pendwa zaidi kwenye wimbo huo, hasa unajiuliza wanakwama wapi.

@lordeyesmweusi ameachia wimbo unaitwa kitanda kampa shavu Gigy Money,unamkuta Gigy Money mwingine kabisa. Kwa Mujibu wa Lord Eyes anadai hizo vocal za Gigy kwenye wimbo huo ni freestyle yani hakuandika popote pale aliposikia beat akapita nalo.

Hii leo neno video vixen kwa @luludivatz halipo kabisa,anasimama kama muigizaji na muimbaji sababu kaamua kuwa serious kwenye angle hiyo hapo.

Game inawasubiri muwe serious muokote pesa zenu


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz