Album ya Ali Kiba Kiboko Yaingia Top Ten Apple Music - EDUSPORTSTZ

Latest

Album ya Ali Kiba Kiboko Yaingia Top Ten Apple Music


Moja kati ya album iliyowahi kumpa mafanikio makubwa msanii Alikiba, ni Cinderella, ambayo aliichia mwaka 2008, ambayo ilifanya vizuri sokoni na kuweka rekodi ya kupata mauzo makubwa, ambayo pia ilimtangaza zaidi na kumfungulia njia mkali huyo.

Kiba alichia album ya pili mwaka 2009 ambayo aliipa jina la Ali k 4 Real, ambayo ilikuwa na ngoma kali kama vile ‘Nakshi Mrembo’, ‘Nichuum’ na ‘Usiniseme’ ambavyo viliwateka mashabiki wa muziki wa BongoFlava, lakini ikashindwa kuvunja rekodi ya Cinderella, ambayo imeendelea kuishi.

Oktoba 7, 2021 (Usiku wa kuamkia leo) msanii Alikiba ameachia album yake ya tatu aliyoiita Only One King, yenye jumla ya ngoma 16. Tayari album hiyo ndani ya saa 15 tangu iachiwe rasmi imeshafanya makubwa kiasi cha kutabiriwa kuja kuvunja rekodi ya Cinderella.

Album hiyo mpya, imefanikiwa kupata mapokezi makubwa kupitia digital platforms mbalimbali, kubwa zaidi imeingia kwenye top Albums za mtandao wa Apple Music duniani kote, ikikamata namba MOJA huku ikizipiku album kama Expensive Pain ya rapper Meek Mill kutoka Marekani na Certified Lover Boy ya Drake.

Una maoni gani, je itavunja rekodi ya Cinderella?? Nini mtazamo wako.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz