elru87tYGBGEm Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Akatwa Mkono na Mumewe Kisa Wivu wa Mapenzi - EDUSPORTSTZ

Latest

Mfanyakazi wa Benki ya CRDB Akatwa Mkono na Mumewe Kisa Wivu wa Mapenzi
Mkazi wa Bushushu mjini Shinyanga, Debora Rwekwama (34) amekatwa mkono wa kushoto na mumewe, Jacob Mwajenga (35) ikidaiwa ni kutokana na wivu wa mapenzi.
Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga, George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9, 2021 mtaa wa Bushushu manispaa ya Shinyanga.

Amesema mwanaume huyo alimkata mkono Debora baada ya mwanamke huyo kuzimia kwa kipigo.

"Inadaiwa mwanaume huyo mchana alikwenda benki (inayodaiwa mkewe kufanya kazi)hakumkuta mkewe lakini alikuta mkoba wake katika ofisi na aliporejea alitaka kuanzisha vurugu lakini wakamshauri ugomvi wao wakaumalize nyumbani."

"Walipofika nyumbani waliendelea na ugomvi na alimpiga sana mkewe hadi akazirai. Alichukua kisu na kumkata mkono inaonekana zilitoka damu nyingi. Mkewe akiwa amezimia huyu mwanaume alimbeba na kumpakia kwenye gari na kwenda wilayani Kahama katika kituo cha polisi na kuripoti kuwa amepata ajali. Kwa sababu Debora alikuwa hawezi kuongea hawakumhoji huhu mwanaume walimpa PF 3 ili aweze kutibiwa lakini hawakujua kama ni mke wake."

"Alipomfikisha hospitali madaktari walifanya uchunguzi wao na kugundua kuwa hajapata ajali bali amepigwa na walitoa taarifa polisi wilaya ya Kahama ambao walimkamata mhusika ambaye shughuli yake ni kuongoza watalii huko Arusha na kutokana na changamoto ya corona alikuwa nyumbani tu, nadhani ndio wivu ulipoanzia hapo, "amesema Kyando.

Amesema Debora amelazwa hospitali ya Wilaya ya Kahama na hali yake ni mbaya, " tunamshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi."

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz