elru87tYGBGEm Nay wa Mitego "Nilishawahi Mkunja Baba Yangu Mzazi na Kumtembezea Kichapo cha Nguvu" - EDUSPORTSTZ

Latest

Nay wa Mitego "Nilishawahi Mkunja Baba Yangu Mzazi na Kumtembezea Kichapo cha Nguvu"
Msanii @naytrueboytz amedai wimbo wa mwanamke hapigwi ni wimbo uliotokana na kisa kilichotokea nyumbani kwao. Nay amedai Dingi yake wa kufikia (Mwanajeshi mstaafu) ni mtu ambaye alikuwa anampiga sana Mama mzazi wa msanii huyo tena muda mwingine anampiga bi mkubwa na mikanda kitu ambacho kilikuwa kinamkwaza sana Nay.

Kuna siku Nay aliona ni muda sasa wa kumnyoosha huyu mzee yani ile "Mnyoosha Hunyooshwa" alipojichanganya kumpa kisago Bi mkubwa ndio muda ambao Nay alipoamua kutembeza kichapo kwa Dingi hadi Dingi akamsalimia mtoto "shikamoo baba"😁😁

Ni kitu ambacho Nay kilimchukiza ila hata mama Mzazi hakupenda kitendo cha Nay kumpiga baba yake ila Nay alifanya vile maana alikuwa anaumia kuona bi mkubwa wake kawa mtumwa wa kipigo kila leo. Hapo ndipo Idea ya wimbo wa Mwanamke Hapigwi uliotoka miaka kumi nyuma ilipopatikana.

Nay anadai yeye na ubabe wake wote na ukorofi wake wote,hajawahi nyanyua mkono kumpiga Mwanamke hata haudhike vipi.

Tangaza Biashara yako nasi piga simu 0714604974 upate offer nzuri

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz