elru87tYGBGEm Mbwana Samatta Atupia Moja Huku Timu yake Ikifungwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Mbwana Samatta Atupia Moja Huku Timu yake Ikifungwa


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ameifungia timu yake, Royal Antwerp ikichapwa 2-1 na wenyeji, Olympiakos katika mchezo wa Kundi D UEFA Europa League Uwanja wa Georgios Karaiskáki Jijini Piraeus, Ugiriki.
Samatta alifunga bao ambalo lilikuwa la kusawazisha dakika ya 74 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Mbelgiji Benson Manuel Hedilazio baada ya mshambuliaji Mmorocco, Youssef
El-Arabi kuwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 52 na kabla ya beki wa kimataifa wa Moldova, Oleg Reabciuk kufunga la ushindi dakika ya 87.
Hizo zilikuwa mechi za kwanza za makundi UEFA Europa League msimu huu na Royal Antwerp itashuka tena dimbani Septemba 30 kuwakabili Eintracht Frankfurt ya Ujerumani nyumbani, Uwanja wa Bosuilstadion mjini Deurne.
Kabla ya hapo watakuwa na mechi tatu za ligi ya nyumbani dhidi ya RFC Seraing Jumapili, Genk Septemba 22 na Union Saint-Gilloise Septemba 26.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz