Mzazi Adai Alipwe Dola Milioni 1 Baada ya Binti yake Kukatwa Nywele na Mwalimu Shuleni - EDUSPORTSTZ

Latest

Mzazi Adai Alipwe Dola Milioni 1 Baada ya Binti yake Kukatwa Nywele na Mwalimu Shuleni
Baba mmoja anadai alipwe dola milioni 1, baada ya binti yake mwenye umri wa miaka 7 kukatwa nywele na mwalimu wake. Jimmy Hoffmeye raia wa Marekani anaishitaki shule ya mtoto wake pamoja na wafanyakazi wake wawili kwa kukata nywele za binti yake bila ruhusa ya mzazi.Kulingana na mashitaka yake, Jimmy Hoffmeyer anasema haki ya mtoto wake ya kuwa na nywele ilikiuka na ameamua kumtoa mtoto wake katika shule hiyo.

Uchunguzi uliofanya kuhusiana na kisa hicho, ulibaini kuwa licha ya kumnyoa nywele, mwalimu huyo pia alimbagua kwa misingi ya rangi yake.

Mwalimu huyo alipatikana na hatia lakini aliendelea kufanya kazi katika shule ya Ganiard iliyopo Michigan. Mashitaka dhidi ya shule na wafanyakazi wake wawili kumuhusi msichana Jurnee yalipelekewa katika Mahakama ya Michigan.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz