Lulu Michael "Sikuwahi Fikiria Kama Nitakuja Olewa na Mtu Mwenye Watoto nje na Mwanamke Mwingine" - EDUSPORTSTZ

Latest

Lulu Michael "Sikuwahi Fikiria Kama Nitakuja Olewa na Mtu Mwenye Watoto nje na Mwanamke Mwingine"


Kupitia InstaStory staa wa Filamu nchini Tanzania @elizabethmichaelofficial amefunguka kuwa haikuwa ndoto yake kuanza maisha na mwanaume ambaye tayari anamtoto na mwanamke mwengine


Lulu amefunguka hayo wakati akimpa ushauri shabiki yake ambaye amerudiana na mpenzi wake wa zamani na kumkuta tayari anamtoto


Lulu ameandika kuwa "Mimi kwenye maisha yangu sikuwahi kutamani kuanza familia na mtu mwenye mtoto tayari. Lakini nikaja kugundua kuwa binadamu hatujakamilika. Wakati mwengine sio mpaka uwe kilema ndio uonekane haujakamili kuna mambo mengine yanaweza kusimama kama kilema. Hili la kuwa na mtoto kabla ya ndoa linaweza kusimama kama kilema"

Lulu akaendelea kwa kuandika lazima ujiulize maswali haya kabla ya kuamua kuwa na mtu mwenye mtoto/watoto tayari. La kwanza "Unampeda?, anakupenda?, anakuheshimu?, Ni mtu anaweza kuwa na wewe kwa kila hali?, Anakusaidia kukusogeza mbele kiakili na kimaisha?, Anakupa furaha na ana support ndoto zako?".

Ameandika hayo Lulu ambaye kwa sasa yupo kwenye ndoa na Mkurugenzi wa EFM na TVE @majizzo ambaye amemkuta na watoto ambao mmoja wapo amezaa na mwanamitindo hamisamobetto
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz