Rayvanny Kumtoa Mwali Leo Huku Harmonize Akifyata Mkia Kumtoa Wake - EDUSPORTSTZ

Latest

Rayvanny Kumtoa Mwali Leo Huku Harmonize Akifyata Mkia Kumtoa Wake


Mwimbaji wa Bongofleva toka WCB Wasafi, Rayvanny anatambulisha wimbo msanii wa kwanza aliyesainiwa chini ya lebo yake, Next Level Music (NLM), Mac Voice.

Kabla ya kusaini NLM, Mac Voice tayari ameshasikika kwenye Bongofleva kwa kipindi cha nyuma ambapo alikuwa chini ya usimamizi wa Chege.

Rayvanny ambaye anakuwa msanii kwanza kuanzisha lebo akiwa bado chini ya WCB Wasafi, ameweka wazi kuwa leo Sepemba 24, 2021 ndipo Mac Voice ataachia ngoma yake ya kwanza.

Leo Ceo wa Konde Gang, Jeshi Harmonize ametangaza kuwa leo Septemba 24 ambapo ilikua ni siku ya kutoa kazi ya kwanza kutoka kwa msanii Cheed maarufu kama 'Cheed Day' imehairishwa.

Harmonize ametangaza hilo kupitia instastory yake akieleza kuwa hakutokuwa na Cheed Day leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

"Siku zote mwenye subira bila shaka yupo karibu na Mungu. Najua kwa kiasi gani mnamsubiri Cheed ila ningependa kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba kwa sababu zilizopo kando ya uwezo wetu Cheed Day haitokuwepo tarehe 24/09/2021 kama tulivyopanga hapo awali. Tunawaahidi kuwajuza lini na siku gani hivi punde" - Harmonize.

Utakumbuka Harmonize naye alikuwa WCB Wasafi lakini akajitoa na kwenda kuanzisha yake ambayo hadi sasa ina wasanii kama Anjella, Ibraah, Killy, Cheed, Country Boy na Young Skales wa Nigeria

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz