Cheed Apata Hofu Kurudi Kwenye Muziki, Harmonize Amtuliza - EDUSPORTSTZ

Latest

Cheed Apata Hofu Kurudi Kwenye Muziki, Harmonize Amtuliza
September 24 ndio siku rasmi ya msanii tokea label ya Konde Gang, @officialcheed kurudi kwenye Game ya Bongo Flava. Msanii huyo amekaa mwaka mmoja na miezi kadhaa bila kutoa Ngoma yake yoyote ile na ukimya huo ulianza toka Mwezi April 2020 alipoondoka rasmi Kings Music pamoja na jamaa yake @officialkilly_tz .

@harmonize_tz kupitia ukurasa wake wa instagram, katusanua kuwa ukimya wa muda mrefu umempa hofu Cheed akiamini atatumia nguvu kubwa sana kusukuma ngoma zake punde tu atavyorudi kwenye game, kitu ambacho Harmonize amedai haiwezi kiwa hivyo maana wakati sahihi ni wa Mungu.

Game imebadilika muda umepita,wasanii wengi wameingia kwenye hili game. Je, Cheed atarudi kama awali au atasanda? Japo binafsi sina shaka nae..,vipi kwa upande wako?

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz