Anayedai Kuwa Mtoto Wa Mzee Yusuf Aibuka; Baba Amenikataa - EDUSPORTSTZ

Latest

Anayedai Kuwa Mtoto Wa Mzee Yusuf Aibuka; Baba Amenikataa
Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Hamad Hassan Mashauri mwenye umri wa miaka 18, mkazi wa Charambe Magengeni jijini Dar es Salaam, ameibuka na kudai kuwa yeye ni mtoto wa mkongwe wa muziki wa Taarab nchini, Mzee Yussuf almaarufu Mfalme.

 

Akizungumza na waandishi wetu, Hamad ambaye pia ni msanii chipukizi wa Singeli, amedai kuwa amewahi kumtafuta Mzee Yussuf na kufanikiwa kukutana naye ana kwa ana lakini tofauti na matarajio yake, mkongwe huyo wa Taarab alimkana hadharani na hata alipoeleza kwamba yupo tayari wakapime DNA, bado aliendelea kushikilia msimamo wake kwamba hamtambui.

 

Waandishi wetu wamefanikiwa kumtafuta Mzee Yussuf na kumhoji kuhusu sakata la kijana huyo ambaye mwonekano wake unashabihiana kwa karibu na msanii huyo mkubwa.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz