elru87tYGBGEm Aliyekuwa Mpenzi wa Beka Flavor Afunguka "Beka Alinifukuza Kisa Ibrah wa Konde Gang, Sikuomba Msamaha" - EDUSPORTSTZ

Latest

Aliyekuwa Mpenzi wa Beka Flavor Afunguka "Beka Alinifukuza Kisa Ibrah wa Konde Gang, Sikuomba Msamaha"Happy muigizaji,mfanya make up na mzazi mwenzie na msanii @bekaflavour1 amedai sababu kubwa ya yeye na Beka kuachana ni kuigiza kwenye wimbo wa @ibraah_tz unaoitwa NIMPENDE uliotoka miezi 7 iliyopita na si kingine.

Happy anadai akiwa location anafanya hiyo video alipigiwa simu na Beka kuwa hasirudi tena nyumbani aishie huko huko,kwa Mujibu wa Beka alidai wakati Happy anaenda kufanya hiyo Video hakuambiwa kuwa atakuwa Video Vixen bali aliaga kuwa anaenda kufanya Make up.

Kitendo cha Happy kuwa Video Vixen kilimkwaza Beka na akaamua kumtimua. Happy anadai hakuomba msamaha kwasababu anamjua Beka ni mtu anayefanya maamuzi magumu na akiamua kufanya maamuzi huwa si mtu wa kuyabadilisha.

Wawili hawa waliwahi patanishwa kwenye kipindi cha LEO TENA cha Clouds Fm na kupewa tiketi za kuhudhuria show ya Mopao Koffi Olomide lakina haikuchukua muda kila mtu akafwata maisha yake. Wakati wakipatanishwa Happy alitaka ndoa ili awe mke halali wa Beka maana anaishi naye bila kuwa na ndoa na ni kurisk maisha yake kwani siku Beka akiamua kumtimua anamtimua tu.

Pia Happy amekiri kuwa Beka anahudumia mwanaye kwa 100% bila tatizo lolote na kwasasa mwanadada huyu anahusishwa kuwa kwenye mahusiano na Othman Njaidi (Patrick Kanumba).


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz