Huenda Dogo Janja Akafunga Ndoa na Huyu Mrembo, Madee Adokeza - EDUSPORTSTZ

Latest

Huenda Dogo Janja Akafunga Ndoa na Huyu Mrembo, Madee Adokeza


Huenda msanii @dogojanjatz yupo mbioni kufunga Ndoa na mchumba wake Queenlina, hii ni kufuatia ujumbe aliouposti msanii @madeeali ambaye ni Baba mlezi wa mkali huyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Jumatano, Septemba 8, 2021.

Kwenye ujumbe huo, Madee awaambia waliokosa ndoa ya Dogo Janja ya kwanza, ya sasa anawapa mualiko.

“Ile ya mwanzo mlinilaumu sana ooh haujatualika, mkatia nuksi mpaka wakaachana... haya hii ya sasa hivi nawaalika tar 15 mwanangu anajambo lake lingine..😂” - Unasomeka ujumbe wa Madee kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Itakumbukwa, Ndoa ya kwanza ya msanii @dogojanjatz alifunga na mrembo Irene Uwoya, Novemba 2017. Ndoa hiyo ilighubikwa na usiri mkubwa katika kufungwa kwake ingawa tetesi za wawili hao kuwa kwenye mahusiano tayari zilikuwepo.

Septemba 2018 taarifa za kuachana kwao zikaanza kuchukua nafasi hasa kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, ndoa hiyo ilikuwa ni ndoa ya pili kwa Irene Uwoya kuvunjika ambapo hapo awali alikuwa ameolewa na mcheza soka, Hamad Ndikumana ambaye kwa sasa ni marehemu.






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz