elru87tYGBGEm Sakata la Picha ya Paula, Rayvanny Aingilia Kazi Ampigia Simu ya Mkwala Shebby Love - EDUSPORTSTZ

Latest

Sakata la Picha ya Paula, Rayvanny Aingilia Kazi Ampigia Simu ya Mkwala Shebby LoveMara baaday ya Msanii wa Bongo Fleva, Shebby Love kutumiwa ujumbe mbalimbali ukimtaka kufuta picha ya mtoto wa muigizaji maarufu Bongo, Kajala Masanja ambaye ni Paula, ameweka wazi kuwa hamuogopi yoyote kwani hakuna kibaya alichokifanya.

Shebby amesema kuwa, alipigiwa simu na msanii Rayvanny ambaye kwa sasa ni mchumba wa Paula akimuhoji kwanini amefanya hivyo lakini, amedai kuwa msimamo wake utabaki kama ilivyo na kwamba, hafuti hiyo picha kwani hamtambui kama ni mtoto wa Kajala.

“Baada ya kusambaa kwa ile ‘cover’ ya nyimbo yangu mpya ya ‘Kitu’ niliona simu ya Rayvanny akuiniambia kuwa, yuko bize na majukumu yake akimaliza atashuhulika na mimi kisa hiyo picha, mwingine ni Kajala aliyenipa masaa 24 niitoe lakini mpaka sasa sijaona akifanya chochote.

“Niseme tu picha iliyotumika mimi naitambua kama katuni na sio mtoto wa Kajala kwahiyo naendelea na muziki wangu,” alisema.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz