Yanga Wametujaribu Wataona cha Mrema Kuni Jiji Litasimama - Simba Waitisha Yanga - EDUSPORTSTZ

Latest

Yanga Wametujaribu Wataona cha Mrema Kuni Jiji Litasimama - Simba Waitisha YangaKlabu ya @simbasctanzania imedai kuwa leo wanasimamisha Afrika huku wakiandika kuwa walijaribiwa na wao sasa wanalipua.

“Mji HAUTOSHI. Tanzania HAITOSHI. Afrika Mashariki HAITOSHI .Leo tunasimamisha AFRIKA . Wametujaribu sisi tunalipua,”- Walichoandika Simba

Kauli hiyo imepokelewa kwa mtazamo tofauti na Mchambuzi wa soka nchini Eddo Kumwembe na kusema kuwa walichogundua ni kuwa timu zote mbili mikwara mitupu.

“Tumegundua timu zote mbili mikwara mitupu,”- @edokumwembe

Hapo jana @yangasc waliandika kuwa siku ya leo jiji litatikisika hata hivyo wakamtambulisha Makambo pengine ilikuwa kinyume na matarajio ya wapenzi wa soka ambao huwenda walidhani ni Banda kama stori za mtaani.

“KESHO JIJI LITASIMAMA!”- Kilichoandikwa na Yanga hapo jana

Kumekuwa na tetesi kwenye mitandao ya kijamii kuwa Peter Banda aliyehusishwa kujiunga na #simbasc huwenda akawa amenaswa na Wananchi, ndiyo maana kiti cha Simba kilibaki kitupu kutwa nzima tangu kilivyo postiwa kama ishara ya kutambulisha mchezaji. Kwa mitazamo hiyo kutoka kwa mashabiki wa soka kumezua hamasa kubwa kujua ni nyota gani atatambulishwa kila linapokuja swala la kutambulisha wachezaji kutoka katika timu hizi za Kariakoo.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz