Unaambiwa Mbunge wa CCM aliyejiuzulu afunguka Makubwa - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaambiwa Mbunge wa CCM aliyejiuzulu afunguka Makubwa



Mbunge aliyejiuzulu afunguka
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa Jimbo la Konde visiwani Zanzibar lipo wazi na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa hivi karibuni. Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dk Wilson Mahera kupitia taarifa yake kwa umma jana.

Dk Mahera alisema NEC ilipokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikitaarifa kuwa, Mbunge Mteule wa Jimbo la Konde, Sheha Mpemba Faki, alikitaarifu chama hicho kuwa hayupo tayari kuwawakilisha wananchi wa Jimbo la Konde kutokana na changamoto za kifamilia.

Alisema kutokana na hilo, NEC inautaarifu umma kuwa jimbo hilo lipo wazi na taratibu za kujaza nafasi hiyo zitatangazwa. “Tume ifanya hivyo kwa kuwa ilikuwa bado haijamjulisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu kukamilika kwa uchaguzi katika Jimbo la Konde na kuchaguliwa kwa Mbunge huyo Mteule. Pia Tume ilikuwa haijamtangaza kwenye Gazeti la Serikali kama ilivyoelekezwa katika Kifungu cha 81 (c) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,” alisema Dk Mahera.

Alisema awali NEC ilipokea taarifa kutoka kwa Spika kuhusu kuwepo kwa nafasi ya ubunge katika Jimbo la Konde lililopo Mkoa wa Kaskazini Pemba kutokana na kufariki dunia kwa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Khatibu Saidi Haji wa Chama cha ACTWazalendo. Dk Mahera alisema kutokana na taarifa hiyo ya Spika, NEC iliitisha uchaguzi uliofanyika Julai 18, mwaka huu.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz