Sarah "Siwezi Rudiana na Harmonize Hata Akiomba Msamaha Tumepeana Block Kila Mahali" - EDUSPORTSTZ

Latest

Sarah "Siwezi Rudiana na Harmonize Hata Akiomba Msamaha Tumepeana Block Kila Mahali"


 
Mwimbaji wa Tanzania Harmonize aliwaacha mashabiki wake kwenye bumbuwazi  baada ya kuomba msamaha hadharani kwa mkewe wa zamani Sarah kwenye akaunti yake ya Instagram.

Wawili hao walikuwa pamoja kwa miaka minne, uhusiano wao ulikuwa wa kupendeza zaidi kati ya wanandoa wengine mashuhuri.

Walienda kwenye hafla pamoja, na pia kuwafanya mashabiki kuwaona wao ni wanandoa kamili.

Baada ya uhusiano wa miaka minne, Sarah alifahamu juu ya mtoto wa siri wa Harmonize ambaye alibarikiwa na mwanamke mwingine bado akiwa kwenye uhusiano naye.


 
Ingawa alimtambulisha binti yake kwa umma na baadaye akaomba msamaha kwa kumficha Sarah, hakusikia yoyotebali waliachana baada ya hayo.

"Samahani ndilo neno pekee naweza tumia kwa mwanamke huyu mrembo 👩 Alienipatia Miaka (4) Ya maisha Yake Nami Nikampatia (4) Yangu Tulipitia Mengi Ila itoshe Kusema Nilizingua Sanaa ..!!! Mpaka Mungu Alipoamua Kuniletea Mtoto Wangu wa Kwanza @zuuh_konde Na Ndo Ikawa Mwisho Wa Safari Yetu Ya Pamoja. Naaam KUTELEZA KUNATOKEA Naa Muungwana Huomba Radhi 🙏 ila Ningeonekana Mjinga Zaidi Ningeendelea Kumficha Mtoto Wangu" Alisema Harmonize.

Baada ya Sarah uona msamha wa Harmonize alimjibu na kusema kwamba hawezi rudiana naye.

"Hata akiomba msamaha siwezi rudiana naye, ndo ni ukweli alifanya vibaya, tumepeana block kila mahali hatuzungumzi naye," Sarah Alisema.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz