Tulihimiza matumizi ya Tiba Asili kwa sababu hapakuwa na njia nyingine ya kupambana dhidi ya Corona - Dkt. Gwajima - EDUSPORTSTZ

Latest

Tulihimiza matumizi ya Tiba Asili kwa sababu hapakuwa na njia nyingine ya kupambana dhidi ya Corona - Dkt. Gwajima




Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameweka wazi kuwa Serikali ya Tanzania ilihimiza matumizi ya tiba asili wakati wa mlipuko wa wimbi la kwanza la Corona kwa kuwa zilionesha kuwasaidia watu wengi kwenye kipindi hicho ambapo Dunia haikuwa na njia mbadala yoyote ya kupambana dhidi ya Corona ukilinganisha na uwepo wa chanjo katika kipindi hiki.

Dkt. Gwajima amesema hayo wakati akiongea na Waandishi wa habari wa nchini Kenya ambapo wamefanya mkutano wa pamoja wa kujadili changamoto zinazowakabili nchi hizo mbili ikiwemo ya UVIKO-19 kwa upande wa mipakani.

“Ugonjwa huu uliingia Wuhan nchini China Disemba 2019, wakati Dunia ilikuwa haielewi ifanye nini, Dunia nzima ilikuwa haina chanjo, haina formula ya dawa, haielewi ifanye nini kwa mfano; wakati huo nyoka ameshaingia ndani na wewe ndio mama na Watoto wamekuzunguka na nyoka yupo mlangoni, inatakiwa unapigana kwa mwiko kwa kummwagia uji au kwa chochote na ndivyo ilivyokuwa ” alisema

Aliendelea kusema kuwa, Tiba asili Kwa upande wa Tanzania lipo Baraza la kitaalamu kisheria ambayo imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kiasi kikubwa zimeonesha kusaidia watu wenye matatizo ya kifua kwa kuona umuhimu katika mapambano hayo ilikuwa ni muhimu kutumia tiba hizo ili kunusuru maisha ya Watanzania.

Hata hivyo Dkt. Gwajima amesema kuwa, Tiba asili zilikuwepo toka zamani kabla ya dawa nyingine hazijaja, na zilisaidia kutibu magonjwa mengi, hata katika vita dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Corona kwenye wimbi la kwanza tiba asili ilionesha mafanikio makubwa sana.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa, licha ya kutumia tiba asili katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona, Serikali ilihimiza wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga nyingine ikiwemo kufanya mazoezi, kula chakula bora (lishe bora), kuvaa Barakoa, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuepuka misongamano isiyo yalazima.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz