Kumekucha..Mbowe na Wenzake Wafikishwa Kisutu - EDUSPORTSTZ

Latest

Kumekucha..Mbowe na Wenzake Wafikishwa KisutuDar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kukiwa na ulinzi mkali.

Washtakiwa hao wamefikishwa Mahakamani hapo saa leo Ijumaa, Agosti 6, 2021 muda wa 2:12 wakiwa kwenye basi dogo la Magereza likisindikizwa na magari mawili ya wazi yenye askari magereza wenye silaha za moto.

Baada ya kuwasili washtakiwa wote walishuka na kuelekea kwenye mahabusu ya Mahakama.


Soma Pia: Lemutuz "Kitendo Cha Tajiri na CEO Wake Kumu Unfollow Haji Manara Kimenikera Sana Sikutegemea Kama Wana Roho nzito Kiasi Hicho"

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Halfani Bwire, Adam Kasekwa na Mohamed Lingwenya.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama na kutenda kosa na kutoa fedha kwa ajili ya kufadhili shughuli za ugaidi.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz