TIMU ya Barcelona imekubaliana na mshambuliaji Lionel Messi kwa kumpa mkataba mpya - EDUSPORTSTZ

Latest

TIMU ya Barcelona imekubaliana na mshambuliaji Lionel Messi kwa kumpa mkataba mpyaTIMU ya Barcelona imekubaliana na mshambuliaji wa timu hiyo, Lionel Messi kwa kumpa mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo.

Barcelona na Messi wamekubaliana kusaini mkataba wa miaka mitano, ikiwa ina maana kuwa mshambuliaji huyo ambaye ameanzia soka lake Barcelona basi atamalizia hapo.Taarifa kutoka Hispania, inasema kuwa Barcelona na Messi wamekubaliana kwenye mkataba huo baada ya Messi kukubali kupunguza mshahara wake.

Mchezaji huyo mwenyeumri wa miaka 34, anatarajiwakumaliza mkataba wake Barcelona akiwa na miaka 39 na
taarifa zinasema kuwa baada ya hapo atastaafu kucheza soka.Pamoja na Messi kukubali kupunguza mshahara wake,

akini bado Barcelona, wanatakiwa kupunguza matumizi mengine ili mchezaji huyo aweze kuingizwa
kwenye listi ya wachezaji wa timu hiyo.

Taarifa iliyoandikwa na Gazeti la Daily Mail, imesema kuwa rasmi mchezaji huyo atasaini mkataba na Barcelona mwishoni mwa wiki hii na ataanza mazoezi rasmi wiki ijayo.

 

Inaonekana kuwa mshambuliaji huyo kwa sasa atakuwa akichukua mshahara wa pauni 250,000 kwa kila wiki.Staa huyo amekaa Barcelona
kuanzia mwaka 2000, amecheza michezo 778 na kufunga mabao 672.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz