Bwana Harusi na Wageni Wake Wauawa na Radi - EDUSPORTSTZ

Latest

Bwana Harusi na Wageni Wake Wauawa na Radi





Radi nchini Bangladesh imewapiga na kuwaua wageni 17 waliohudhuria sherehe ya harusi moja nchini humo. Watu 14 wengine ikiwemo bwanaharusi , walijeruhiwa . Wakati huo bi harusi hakuwepo katika sherehe hiyo.

 

Sherehe hiyo ilikuwa inafanyika katika boti moja katika mji uliopo karibu na mto wa Shigbanj, wakielekea katika nyumba ya biharusiwakati walipopigwa na radi hiyo. Wakazi wanasema kwamba radi kadhaa zilipiga kundi hilo.

 

Kila mwaka mamia ya watu kusini mwa bara Asia hufariki kutokana na radi. Mwaka 2016, Bangladesh ilitangaza radi kuwa janga wakati zaidi ya watu 200 walipofariki katika mwezi wa Mei pekee, ikiwemo watu 82 katika siku moja.

 

Wataalamu wanasema kwamba kukatwa kwa misitu kumesababisha ongezeko la radi kutokana na kutoweka kwa miti mingi mirefu ambayo huzuia radi.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz