Polisi yamdhibiti aliyefyatua risasi



Dar es Salaam. Mtu mmoja ambaye hajafahamika amezua taharuki maeneo ya Daraja la Salenda, Dar es Salaam, baada ya kufyatua hewani risasi huku akisikika kuwa anawatafuta polisi.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 25, 2021 liliwafanya wananchi waliokuwa jirani na eneo hilo wakiwemo waliokuwa kwenye magari kukimbia kujaribu kuokoa maisha yao.

Hata hivyo, Polisi walifanikiwa kumdhibiti na taarifa ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa, ameuawa kwenye mapambano hayo na polisi.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post