Mopao Kuitikisa Dar Leo, Manara Asimamia Shoo - EDUSPORTSTZ

Latest

Mopao Kuitikisa Dar Leo, Manara Asimamia Shoo




MSANII ambaye anatarajiwa kutumbuiza katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi, Koffi Olomide maarufu Mopao, jana Jumamosi aliwasili Dar na kufanya jiji kutikisika kidogo baada ya wale waliokuwa hawaamini kama atakuja, kumshuhudia live.


Mopao alitua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam ambapo Msemaji wa Yanga, Haji Manara, alisimamia shoo ya kumpokea.Muda mfupi baada ya Mopao kutua, wachezaji wa Yanga na Simba waliokuwa wamebaki Morocco nao walitua.


DJUMA SHABANI AAHIDI FURAHA
Beki mpya wa Yanga, Djuma Shabani, amesema katika Tamasha la Wiki ya Mwananchi linalofanyika leo Jumapili, wapenzi wa Yanga wanatakiwa wasikose kushuhudia burudani kutoka kwao kwa kucheza soka safi.




Akizungumza na Spoti Xtra, Djuma alisema: “Ni furaha sana kuona nipo ndani ya Yanga, hii ni siku muhimu sana kwa Wanayanga wote na wanachotakiwa kufanya ni kuhakisha wanafika kwa wingi uwanjani kuja kuishudia timu yao mpya.“Kwa sisi wachezaji tunaahidi burudani nzuri kwa mashabiki wetu ikiwemo kuibuka na ushindi katika mechi yetu ambayo tutacheza, wachezaji wote wanafikiria hilo kwa sasa na sisi tupo tayari kwa ajili ya mapambano,” alisema beki huyo.


 


MUKOKO KUKOSEKANA
Wakati nyota hao wakirudi kwa ajili ya kushiriki Tamasha la Wiki ya Mwananchi, kiungo wa timu hiy Mukoko Tonombe atakosekana kutokana na asubuhi ya leo kuwa na ratiba ya kusafiri kuelekea DR Congo kujiunga na timu ya taifa.


MAKAMBO: NJOONI NIWAJAZE
Mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo, amesema: “Kila Mwanayanga alikuwa anatamani sana siku hii ifike, wachezaji pia tulikuwa tukiisubiri kwa hamu sana, hivyo mashabiki wanatakiwa kuja kwa wingi ili kuishudia timu yao mpya.“Kwa upande wangu naahidi kuwajaza endapo nitafanikiwa kufunga bao, natamani kufunga, naamini nitafanikiwa katika hilo.”
Yanga inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Zanaco FC ya Zambia




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz