Miquisone Afanyiwa Kufuru Misri - EDUSPORTSTZ

Latest

Miquisone Afanyiwa Kufuru Misri

HABARI ikufikie kwamba, Klabu ya Al Ahly ya Misri, itakuwa inamlipa Luis Miquissone mshahara wa kufuru ambao unatajwa kuwa ni takribani mara nane aliokuwa akipewa ndani ya Simba.


Miquisone ambaye alijiunga na Simba, Januari 2020, tayari ameuzwa na timu hiyo kwenda Al Ahly.Akiwa Simba, kiungo huyo raia wa Msumbiji, alikuwa akipokea zaidi ya shilingi milioni nane kwa mwezi, lakini huko Al Ahly atapokea zaidi ya shilingi milioni 60.

 

Chanzo kutoka ndani ya Simba, kimelieleza Spoti Xtra kwamba, pamoja na Simba kunufaika na pesa ya uhamisho wa kiungo huyo, jambo lililomvutia Miquisone kwenda Al Ahly ni mshahara aliotangaziwa na Waarabu hao.

 

“Ujue watu wengi hawajui kisa cha mabosi wetu Simba kuamua kumuuza Miquissone, huyu mchezaji kaiingizia klabu yetu takribani shilingi bilioni mbili.“

 

Uhamisho wake ulitokana na ushawishi alioupata baada ya kuwekewa mshahara mnono ambao ni zaidi ya mara nane aliokuwa akipewa na Simba, hivyo akajikuta anaomba uongozi umruhusu kuondoka.“Hivyo kama viongozi hawakuwa na budi kumruhusu maana hata kama wangemkatalia kulikuwa na uwezekano mkubwa baadaye kuondoka bure au kwa dau dogo,” kilisema chanzo chetu.

Stori: MUSA MATEJA, Dar es Salaam
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz