IGP Sirro atoa msimamo kukamatwa kwa Askofu Gwajima. - EDUSPORTSTZ

Latest

IGP Sirro atoa msimamo kukamatwa kwa Askofu Gwajima.
Baada ya Waziri wa Afya Dkt.Doroth Gwajima kuagiza Jeshi la Polisi na TAKUKURU kumkamata Askofu Josephat Gwajima na kumuhoji kwa tuhuma za kupotosha juu ya Chanjo ya UVIKO-19, hatimaye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema wanachokisubiri sasa ni maelekezo ya maandishi kutoka kwa Waziri huyo.

"Tumeyasikia hayo maelekezo, jambo la msingi unajua maelekezo ya kiserikali mara nyingi yanakwenda kwa maandishi, tunasubiri maandishi ya kuonyesha kuna kosa gani, maanake sisi tunashughulika na makosa ya jinai, kwahiyo nasubiri maelekezo kutoka kwake alafu tutaangalia kama ni makosa ya jinai tutachukua hatua na kama tutaona ni vinginevyo tutashauri njia nyingine itumike badala ya kutumia Jeshi la Polisi"-IGP-Sirro.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz