Malawi: Waziri wa zamani akamatwa kulipa gharama za fungate kwa fedha za Umma - EDUSPORTSTZ

Latest

Malawi: Waziri wa zamani akamatwa kulipa gharama za fungate kwa fedha za Umma
Waziri wa zamani wa Malawi amekamatwa kwa kwa madai ya kulipa gharama za fungate kwa kutumia pesa za Umma.Charles Mchacha, aliyekuwa waziri wa umwagiliaji wakati wa utawala wa Rais wa zamani Peter Mutharika, anadaiwa kutumia fedha za wizara kwa ajili ya kugharamia hoteli ya hadhi ya juu kwa ajili yake na mkewe baada ya harusi mjini Blantyre.

Gazeti la Nation la Malawi liliandika kwenye ukurasa wa twitter kuwa maafisa wengine wawili wa serikali pia wamekamatwa na taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo.

BREAKING: Anti-Corruption Bureau (ACB) has arrested former Minister of Irrigation and Water Development, Charles Mchacha, Principal Secretary for Ministry of Irrigation and Water Development, Henrie Njoloma and Moses Mwenye, Acting CEO for Lilongwe Water Board. 
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz