Gerson Msigwa: Mapato kutokana na Bandari yameongezeka kutoka shilingi bilioni 525.4 hadi shilingi bilioni 531 - EDUSPORTSTZ

Latest

Gerson Msigwa: Mapato kutokana na Bandari yameongezeka kutoka shilingi bilioni 525.4 hadi shilingi bilioni 531
“Mapato kutokana na Bandari yameongezeka kutoka shilingi bilioni 525.4 hadi shilingi bilioni 531, bandari zetu zimeendelea kufanya vizuri licha ya changamoto za Ugonjwa wa Uviko-19 duniani” “Bandari yetu ya Dar es Salaam wiki tatu zilizopita imeandika rekodi kubwa kwa Bara la Afrika, ambapo kupitia gati maalumu ilifanikiwa kupokea magari 3743, na asilimia 65 ya magari hayo (magari 2945) yalikuwa yanapelekewa nje ya nchi”

“Hadi kufikia mwezi Machi, 2022 Bandari ya Karema itaanza kufanya kazi, hali itakayopelekea kupanua wigo wa usafirishaji mizigo kwenda nje ya nchi”
“Serikali imewekeza Bilioni 600 katika mkongo wa Mawasiliano wa Taifa ili kutoa huduma na kuleta nafuu kwa watumiaji wa huduma za simu ikiwemo kupiga na data. Watoa huduma wote wa simu nchini wanahudumiwa na mkongo huu, na mkongo huu unasimamiwa na
@TTCLCorporation 
ili kupeleka huduma ya mawasiliano katika maeneo ambayo hayana mawasiliano hapa nchini”

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz