Makambo: Nimekuja Kuchukua Makombe - EDUSPORTSTZ

Latest

Makambo: Nimekuja Kuchukua Makombe

“NIMEKUJA kufanya kazi.” ndilo neno pekee ambalo amelisema mshambuliaji mpya wa Klabu ya Yanga, Heritier Makambo tena kwa msisitizo mkubwa, muda mfupi baada ya kusaini mkataba na kutambulishwa kuwa mchezaji mpya wa klabu hiyo.

 

Makambo amerejea katika kikosi cha Yanga baada ya kufikia makubaliano ya kuachana na Klabu ya Horoya ya Guinea, aliyojiunga nayo mwaka 2019 kufuatia changamoto za uhusiano wake na kocha wa timu hiyo.

 

Nyota huyo inaelezwa kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Yanga.Akiwa na Yanga msimu wa mwaka 2018/19 Makambo aliifungia klabu hiyo mabao 17, na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye chati ya wafungaji bora kinara akiwa, Meddie Kagere wa Simba aliyetupia mabao 23 kisha Salim Aiyee ambaye ni mzawa alikuwa nafasi ya pili kwenye chati ya ufungaji.

 

Alipoombwa kuzungumza chochote baada ya utambulisho huo, Makambo hakutaka kuwa na maneno mengi ambapo alisema kwa kifupi: “Siwezi kuzungumza kitu kwa sasa zaidi ya kuwaahidi Wanayanga kuwa nimekuja kufanya kazi, na kuisaidia Yanga kushinda makombe.

 

”Makambo aliyatamka maneno hayo mbele ya Injinia Hersi ambaye pia alizidi kumsisitiza kuhusiana na umuhimu wa kuwarejeshea Wanayanga furaha.

 

Naye Kaimu Katibu mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa alizungumza mambo mbalimbali kuhusu usajili unavyokwenda klabuni hapo.

 

“Bado hatujamaliza usajili, tutaendelea kushusha majembe mapya kutoka nje ya nchi lakini pia, nyota mbalimbali wazawa katika malengo ya kuhakikisha tunakuwa na kikosi bora zaidi na imara kwa msimu ujao.“

 

Wapo wachezaji tunaohusishwa nao lakini nisingependa kuzungumza hayo kwa sasa, tutawaweka wazi pale kila kitu kitakapokuwa tayari.

“Kwetu malengo makubwa ya kufanya usajili huu ni kuhakikisha tunarejesha furaha ya mashabiki wa Yanga, kwa kushinda makombe katika michuano ambayo tutashiriki mwakani.“

 

Kila mnachokiona katika usajili huu ni mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi, tunataka mpaka atakaporudi akute ripoti aliyoiacha imekamilika, lakini pia tumekuwa tukimuhabarisha katika kila hatua ambayo tumefikia.”

NA JOEL THOMAS, Dar es Salaam
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz