Fahyma Avunja Ukimya kwa Ibraah na H Baba "Mnikome" - EDUSPORTSTZ

Latest

Fahyma Avunja Ukimya kwa Ibraah na H Baba "Mnikome"

 


Mama wa mtoto wa msanii Rayvanny, Fahyma Fahyvanny amevunja ukimya kwa kile kinachoendelea mitandaoni kwa wasanii Ibraah wa Konde Gang na H Baba kupost picha zake kwenye page zao za Instagram.

Fahyvanny amesema hataki mazoea ya kijinga na sheria itafuata mkondo wake kwa wanaotumia jina lake na picha yake kwa manufaa yao binafsi.

"Naomba ifike mahali muda muwe na heshima na jina la mtu, unayetumia picha yangu na jina langu kwa manufaa yako sheria itafuta mkondo wake, nipo kimya sitaki mazoea ya kijinga, kwa kuongezea naomba jina langu au picha zangu zisitumike kwenye mambo ya drama 'I’m not a drama queen' naomba nisihusishwe na ujinga wa aina yoyote ule tafadhali" 

"Naomba nieleweke sina mahusiano na yeyote, anayetumia picha zangu nadhani nimeeleweka ikiendelea hii tutapelekana pabaya, maana nimekaa kimya sio kwamba sioni ila nimeongea kukanusha mambo ya kijinga, mimi ni mtu na heshima zangu hivyo nisitumike kijinga tafadhali" ameongeza 

Wasanii Ibraah na H Baba kwenye siku za hivi karibuni wamekuwa wakitumia picha za mrembo huyo kwa kupost kwenye page zao za Instagram.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz