EWURA yasikia kilio cha wananchi kuhusu gesi - EDUSPORTSTZ

Latest

EWURA yasikia kilio cha wananchi kuhusu gesiMamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewaagiza wafanyabishara kusitisha mara moja upandishwaji wa bei ya gesi ya kutumia majumbani na badala yake warudishe bei ya awali hadi pale itakapopokea na kupitia mapendekezo na uhalali wa wao kupandisha bei.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Mamlaka hiyo Titus Kaguo, wakati akizungumza kwenye kipindi cha DriveShow cha East Africa Radio.

"Gesi haishikiki na tumekuja kugundua wafanyabiashara hawa wamepandisha bei kiholela kuna utaratibu haujafuatwa na watu wameanza kulalamika, tulichofanya tumewaagiza warudishe bei walizokuwa wanatumia kabla hawajapandisha," amesema Kaguo

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz