Chidi Benz Amfunza Haji Manara "Riziki Anatoa Mungu sio Mo Dewji Wala Barbra" - EDUSPORTSTZ

Latest

Chidi Benz Amfunza Haji Manara "Riziki Anatoa Mungu sio Mo Dewji Wala Barbra"

 


Rapa Chidi Benz King Kong ameshea comment yake kwa Haji Manara baada ya kumaliza 'press' yake na waandishi wa habari kwa kumkaribisha Manara katika klabu ya Yanga kwani riziki anaotoa Mungu na sio Mohammed Dewji au Barbara Gonzalez.

"Kaka yangu Haji Manara nakukumbusha tu riziki apangae ni mwenyezi Mungu, sio Mohammedi au Barbra na kila hatua dua, you never know Mungu anakuepusha na nini na mbele kakupangia nini, shukuru kwa yote and calm down"

Chidi Benz ameongeza kuwa "Mlango mmoja ukifungwa mwingine uko wazi karibu Yanga kwa baba yako, ulitukera sana lakini mtoto akinyea mkono haukatwi, welcome back home".

Aidha msanii wa filamu Vincent Kigosi yeye ameandika kuwa "Ndugu yangu Manara kwenye kila ajira kuna changamoto na ni vyema kuondoka sehemu vizuri unaweza rejea tena"


Naye raisi wa BongoFlava na mtangazaji wa PlanetBongo ya East Africa Radio Dullah Planet pia ameandika kwamba popote alipo Haji Manara naye yupo upande huo.


Sakata la Haji Manara kuacha kazi Simba limezua sura mpya baada ya maneno aliyoyazungumza kwenye press yake dhidi ya waandishi wa habari.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz