Wanajeshi wa kike kuvaa ‘Skuna’ wakati wa gwaride Ukraine, mjadala waibuka - EDUSPORTSTZ

Latest

Wanajeshi wa kike kuvaa ‘Skuna’ wakati wa gwaride Ukraine, mjadala waibuka

 


Mipango ya Wizara ya ulinzi ya Ukraine kuruhusu wanajeshi wa kike kupiga gwaride wakiwa wamevaa skuna badala ya viatu vya kijeshi kwenye gwaride mwezi ujao imezua ghadhabu.

Iryna Gerashchenko, mbunge wa upinzani amesema, uamuzi huo ni unyanyapaa wa kijinsia, na si usawa wa kijinsia.

Ukraine inajiandaa kwa gwaride la jeshi tarehe 24 mwezi Agosti kuadhimisha miaka 30 ya uhuru tangu kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti.

Wizara ya ulinzi inasema viatu ni sehemu ya sare.

Watu nchini Ukraine wameeleza kushtushwa kwao, huku kundi la wabunge wakimtaka Waziri wa ulinzi Andriy Taran kuomba radhi.

”Habari ya gwaride kupigwa huku wakiwa wamevalia skuna ni jambo la fedheha,” alisema mtangazaji Vitaly Portnikov kwenye mtandao wa Facebook.

Bi Gerashchenko alisema mwanzoni alifikiria wanajeshi wanawake wakifanya mazoezi katika suruali za kijeshi na viatu vyenye visigino virefu huo ni uongo, na alishangaa ni kwanini wizara ilidhani visigino ni muhimu zaidi kuliko kubuni silaha za mwili zinazolingana na wanawake.

Maria Berlinska, mwanajeshi mkongwe alisema gwaride linapaswa kuonesha umahiri wa kijeshi.

Olena Kondratyuk, naibu spika wa bunge, alisema kuwa zaidi ya wanawake 13,500 walikuwa walipambana katika mzozo wa sasa unaowakabili Ukraine dhidi ya wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Urusi eneo la mashariki.

Zaidi ya wanawake 31,000 sasa wanahudumu katika jeshi la nchi hiyo, wakiwemo zaidi ya 4,000 ambao ni maafisa.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz