Ni Kweli Diamond Platumz na Wasafi Hununua Viewers? Kwa Kitendo Hichi Wasafi Wakubali Automatic Kuwa Wasanii Wananua viewers - EDUSPORTSTZ

Latest

Ni Kweli Diamond Platumz na Wasafi Hununua Viewers? Kwa Kitendo Hichi Wasafi Wakubali Automatic Kuwa Wasanii Wananua viewers



Ameandika Leak/JF

Wasafi Fm kupitia ukurasa wao wa instagram waliweka maneno ya msanii kutoka Nigeria ambaye alikuwa anasema kuwa wasanii waache kununua viewers wa youtube na akasisitiza kuwa anawambia wasanii wengine sio wanigeria maana wa uko Nigeria awawezi kununua viewers wa Youtube.

Kwenye hili sikubaliani nae msanii husika kwani kama kweli kuna utapeli wa kununua watazamaji youtube basi ni ngumu kuamini wasanii wa Nigeria washindwe kununua viewers kwa walivyo hodari kwa utapeli.

Baada ya msanii huyo kuweka hiyo post wengi wakiwemo wasafi media waliweka hiyo post kwenye mitandao yao kwani walikuwa wanaamini anaambiwa Harmonize lakini wakasahau wao walisha ambiwa wananua viewers wakasema haiwezekani kununua viewers youtube. Nini kimegeuza msimamo wao?

Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi wa nne Director Hansacana alisema wazi kuwa wasanii wananunua viewers na akaoneshwa jinsi inavyo wezekana kununua viewers.

Lakini Director huyu alishambuliwa sana wakiwemo wafuasi wa Diamond ambao walisema haiwezekani na wakajitokeza wataalam wakasema haiwezekani kununua viwers na Maneneja wake Diamond na Wasafi walisema wazi kuwa haiwekani kununua viewers na kama inawezekana basi kila mtu anunue na waliendelea mbele na kusema msanii Diamond na wasafi wanaonewea wivu

Baada ya majuma Machache tena Mkurugenzi wa EFM bwana Majizo akihojiwa na Gerald Hando alisema wazi kuwa kuwa msanii kuwa na viewers wengi sio kigezo cha kuwa na wimbo mzuri au kuwa msanii mkubwa kwani kwenye viewers wa youtube kuna siasa nyingi

Baada ya hii kauli Diamond na Mameneja wake walimshambulia sana Majizo wakisema anawaonea wivu wasanii wa wasafi na Diamond kupitia ukurasa wake alionesha na kuandika umuhimu wa viewers na umuhimu wa kuwa na viewers wengi hata hivyo wafuasi wa Diamond na wasafi waliendelea kuwashambulia wote waliosema kuwa wasanii wananunua viewers wakisema ni watu wanao muonea wivu msanii Diamond na hawamtakii mema.

Watu wameshangazwa wasafi kukubaliana hoja ya kununua viewers wakati walikuwa wanapinga vikali kabisa wakisema haiwezekani kabisa sasa tunaanza kujiuliza kwanini wamekubali leo?

Kwa sababu sio Diamond anaye ongoza kuwa na viwers?

Kwa sababu sio wasanii wa wasafi wanao ongoza kwa Viewers uko Youtube?

Kwa sababu Wasafi hawapendi kuzidiwa na wana muhaho?

Kinyago wanacho pambana nacho sasa wasafi walikichonga wenyewe kwa hiyo kama kinyago kina nunua viewers basi kimepata ujuzi wa kununua viewers uko uko wasafi si kwingineko.

Kwa hiyo kwa Muktadha huo Wasafi wanakubaliana nasi kuwa viewers zinaweza kununuliwa? nashutuma juu ya wasanii wao kununua viewers zilikuwa za haki kabisa?

Je, ni kweli Diamond ananunua viewers?





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz