Mange Kimambi "Im an Organ Donor, Meaning Nikifa Watatoa Viungo Vyangu kumpa Mtu Mwingine" - EDUSPORTSTZ

Latest

Mange Kimambi "Im an Organ Donor, Meaning Nikifa Watatoa Viungo Vyangu kumpa Mtu Mwingine"


Reposted from @mangekimambi_ Im an organ donor. Meaning nikifa watatoa viungo kama moyo, figo, ini, kizazi (Uterus), mapafu kadhalika na kumuwekea mtu mwingine.

Hicho kidoti cha pink hapo kwenye leseni ndo kinaonyesha ni mtu ambae nimesha sign makaratasi kuwa nikifa watoe kila kitu waokoe maisha ya mtu mwingine. Mi nizikwe na viguu vyangu vyembamba tu sidhani kama kuna mtu atavitaka 🤣.

I know mambo ya dini and so forth, but mimi ni mama ambae nilishauguza mtoto alipata tatizo la figo. Ni Mungu tu alisaidia akapona completely baada ya kupewa masteroids, Ila sitokaa kusahau Kenzo alivyojaa maji mwili mzima mpaka vipumb* vilijaa maji 😩.Doctor aliniambia kuna mawili, either ni anaweza kupona kabisaaa au akawa na tatizo kubwa mpaka akahitaji figo ingine. Nilianza kuwaza ntapata wapi figo ya mtoto? Nikawaza kuna watoto wanazikwa na figo, why asipewe mwanangu? So in that moment nilimpromise Mungu kuwa mwanangu akipona na mimi nitakuwa organ donor.
Why tunazikwa na hizo organ zinaoza tu badala wapewe wagonjwa wapone?

So hii alama imewekwa kwenye leseni yangu ili hata kama nikipata ajali ya gari na hakuna mtu wa kuwaambia mimi nilikubali kutolewa viungo wao wakiangalia tu leseni wanajua wanaanza kunicharanga charanga 😭😩.

Hiyo video ya pili, ndo kipindi Kenzo anaumwa figo. Nilikuwa nikimpa dawa ( Steroids) ndo analia tumbo linamuuma😭.Aisee pitia yote ila sio kuuguza mtoto.Nilikuwaga naliaaa akianza kulia tumbo linamuuma maana lazma nimpe hizo steroid. Madawa makali mtoto aliota nywele mwili mzima mpaka usoni akawa kama katoto ka nyani, niliachaga na kumposti😩.
Hapo ilikuwa ndo wiki ya pili tumeingia marekani so Kenzo alikuwa anajua kiswahili tu.Ila nashukuru Mungu tatizo alilipatia marekani angelipatia Tz ningezika mtoto maana vipimo vilivyofanyika, teknolojia iliyotumika kwenye vipimo, specialist wa figo za watoto niliepewa,ingekuwa TZ ningezika. Staki kukumbuka.

Moral of the story ni kwamba ingekuwa vizuri wote tukikubali kutolewa viungo tukifa ili tuokoe wagonjwa wanaoweza kupona.Huwezi kuelewa umuhimu wa hili swala hadi yakufike uanze kutafuta moyo au mapafu au figo alafu ukumbuke kuna nyingi zinaliwa na wadudu makaburini.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz