TIMU ya Taifa ya Italy imefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Kombe la Euro2020 baada ya kuifunga Uingereza kwa jumla ya mikwaju ya penati 3-2.
Uingereza ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la mapema kabisa kunako dakika ya pili tu ya mchezo kupitia kwa Luke Shaw baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Koeran Trippier, bao ambalo lilidumu dakika zote 45 za kipindi cha kwanza.
Kunako kipindi cha pili, lilipigwa shambulizi la hatari kwenye lango lango la Uingereza lililozaa matunda kwa Italy baada ya kupata bao la kusawadhisha kupitia kwa Bernardo Bonucci dakika ya 67 na kufufua matumaini mapya ya kuipeleka ndoo hiyo Roma.
Mpaka dakika 90 zinamalizika ubao ulikuwa ni 1-1 ambapo ziliongezwa dakika 30 zilizoisha bila kubadilisha ubao wa matokeo ndipo yakatengwa matuta kutafuta mbabe.
Italy wameshinda penati 3-2 huku wachezaji wao Andrea Belotti na Jorginho (Muingereza mwenye asili ya Brazil) wakikosa penati. Kwa upande wa Uingereza, penati zote za mwisho Marcus Rashford Jadon Sancho na Bukayo Saka wakikosa.
Italy inafikisha mara mbili kushinda kombe la EURO huku ikicheza fainali nne wakati Uingereza haijawahi kuchukua ndoo ya EURO na hii ilikuwa fainali yao ya kwanza ambayo kombe limechukuliwa kwenye ardhi yao ya nyumbani.
Post a Comment