Hiki ndio kikosi cha mamluki kilichomuua rais wa Haiti - EDUSPORTSTZ

Latest

Hiki ndio kikosi cha mamluki kilichomuua rais wa Haiti
Kundi la mamluki 28 wa kigeni, pamoja na wanajeshi wastaafu wa Colombia, walimwua Rais wa Haiti Jovenel Moïse mapema wiki hii, polisi wanasema.Baada ya vita vikali katik mji mkuu Port-au-Prince, 17 walizuiliwa, wengine kwenye nyumba waliyokuwa wakitumia, wengine baada ya kuingia katika eneo la kidiplomasia la Taiwan.

Washukiwa watatu waliuawa na polisi na wanane bado wanatafutwa.

Watuhumiwa waliopatikana nguo zao zikiwa zimeloa damu walikamatwa na walionyeshwa kwa vyombo vya habari Alhamisi, pamoja na silaha hatari wanazodaiwa kutumia .

Axes, wire-cutters, sets of US dollar bills and Colombian passports have been seized
Bado haijulikani ni nani aliyepanga shambulio hilo na kwa nia gani.

Shambulio hilo lilitokea mapema asubuhi ya Jumatano, wakati watu wenye silaha walipovamia nyumba ya rais huko Port-au-Prince, wakimpiga risasi na kumuua na kumjeruhi mkewe. Bw Moïse, 53, alipatikana amelala chali na majeraha 12 ya risasi na jicho lililotobolewa, kulingana na mamlaka.

Martine Moïse, 47, alijeruhiwa vibaya na yuko katika hali nzuri baada ya kusafirishwa kwenda Florida kwa matibabu.

Pasipoti na silaha zanaswa
Polisi walisema kikosi cha mamluki hao ni pamoja na Wakolombia, pamoja na Wamarekani wawili wenye asili ya Haiti.

Miongoni mwa vilivyopatikana kutoka kwa washukiwa ni bunduki, sarafu za dola za kimarekani, kitabu cha hundi kibinafsi cha rais na seva iliyokuwa na picha za kamera za boma la rais , gazeti la Le Nouvelliste liliripoti.

Taiwan ilithibitisha kuwa washukiwa 11 walikamatwa baada ya kuvunja ua na kuwa ndani ya boma la rais huyo.

Raia wenye hasira walikuwa wamejiunga na msako wa watu hao na kusaidia polisi kuwafuata wengine ambao walikuwa wamejificha kwenye vichaka. Umati uliteketeza magari matatu ya washukiwa na kuharibu ushahidi.

“Sisi Wahaiti tunashtuka, hatuikubali,” mtu mmoja aliliambia shirika la habari la AFP. “Tuko tayari kusaidia kwa sababu tunahitaji kujua ni nani aliye husika na hili, majina yao, historia yao ili haki itendeke”

Mkuu wa polisi Léon Charles alitaka utulivu, akisema umma haupaswi kuchukua sheria mikononi mwao.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, polisi walionyesha waandishi wa habari pasipoti za Colombia.

“Wageni walikuja nchini mwetu kumuua rais,” Bwana Charles alisema, wakati washukiwa wakiwa wameketi sakafuni nyuma yake wakiwa wamefungwa pingu.

The crowd reacts near the Police station where armed men are being detained
Serikali ya Colombia imethibitisha kuwa washukiwa wasiopungua sita walionekana kuwa wanachama wastaafu wa jeshi lake. Imeahidi kuisaidia Haiti na juhudi zake za uchunguzi.

Idara ya mashauri ya kigeni ya Marekani, wakati huo huo, ilisema haiwezi kuthibitisha ikiwa raia wake yeyote alikuwa amezuiliwa.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani na Canada vinaripoti kuwa mmoja wa raia wawili waliokamatwa, James Solages, 35, anatoka Florida na alikuwa mlinzi wa zamani katika ubalozi wa Canada huko Haiti.

Jaji anayechunguza kesi hiyo aliambia vyombo vya habari vya eneo hilo kuwa Bwana Solages na raia mwingine wa Marekani , aliyeitwa Joseph Vincent, walikuwa wamesema walikuwa huko kama watafsiri kwa mamluki, baada ya kupata kazi hiyo kwenye mtandao

“Misheni ilikuwa kumkamata Rais Jovenel Moïse … na sio kumuua,” Jaji Clément Noël aliiambia Le Nouvelliste.

Gazeti la El Tiempo la Colombia lilisema kwamba lilikuwa limeona nyaraka za siri ambazo ziliwataja washukiwa wa Colombia. Utafiti wa jarida hilo unaonyesha kwamba wanne kati yao walisafiri kutoka Kolombia kwenda Jamhuri ya Dominika mnamo 4 Juni.

Walivuka kwa ardhi kutoka hapo kwenda Haiti siku mbili baadaye. Nchi hizo mbili zina mpaka wa pamoja wa kisiwa cha Hispaniola.

Mamluki waliomuua rais wa Haiti
Kulingana na El Tiempo, majasusi wa Colombia wameona picha zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii za wanachama wa kikundi hicho, zikiwaonyesha wakiwa katika eneo maarufu la watalii katika Jamuhuri ya Dominika.

Mauaji hayo yamesababisha machafuko ya wenyewe kwa wenyewe nchini Haiti, taifa maskini zaidi katika Amerika. Hali ya hatari bado inatumika kote nchini, wakati Jamhuri ya Dominika imefunga mpaka wake.

Nani anayeongoza nchi?
Mauaji hayo yameleta mkanganyiko juu ya nani aongoze Haiti, angalau hadi uchaguzi ufanyike.

Kanuni katika katiba zimvurugwa wakati huu ambapo hakuna Bunge – mizozo ilimaanisha uchaguzi mnamo Oktoba 2019 haukufanyika – kwa hivyo haiwezi kuchagua rais mwingine.

Marekebisho ya katiba, ambayo hayakubaliwi na kila mtu, yanaonyesha kwamba waziri mkuu anapaswa kuongoza, lakini uhalali wa Bw Joseph unapingwa.

One of a number of cars set on fire during anger over the killing
Mwanasiasa mwingine, Ariel Henry, alikuwa ameteuliwa kama Waziri Mkuu mpya muda mfupi kabla ya mauaji, lakini alikuwa bado hajaapishwa.

UN inasema Bw Joseph anapaswa kuendelea kuwa kiongozi mpaka uchaguzi utakapofanyika baadaye mwaka huu.

Amesema hatogombea urais. “Siko hapa kukaa muda mrefu. Tunahitaji kufanya uchaguzi. Sina ajenda ya kibinafsi,” aliiambia BBC.

Haiti imekuwa ikikumbwa na machafuko ya kisiasa na kiuchumi, na hivi karibuni na ongezeko la vita vya magenge.

Kulikuwa na maandamano yaliyoenea yakitaka kujiuzulu kwa Bw Moïse, ambaye alikuwa akitawala kwa amri tangu uchaguzi ucheleweshwe.

Credit by BBC
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz